Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kimataifa muhimu kukabili changamoto za Sahel: Ban

Ushirikiano wa kimataifa muhimu kukabili changamoto za Sahel: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wanaoambatana naye kwenye ziara huko ukanda wa Sahel akiwemo Rais wa Benki ya dunia, kamishina wa muungano wa afrika, kamishina wa maendeleo wa Muungano wa Ulaya na mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa ushirikiano wa jumuiya ya nchi za Kiarabu OIC wamekuwa na mazungumzo na Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali mjini Bamako Joseph Msami na taarifa kamili

 (RIPOTI YA JOSEPH MSAMI)

 Katika mazungumzo ya viongozi hao  Ban amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto zinazokabili ukanda waSahel. Ban na Rais Keita pia wamejadili hali ilivyo nchiniMaliambapo Katibu Mkuu amesifu maendeleo yalopatikana baada ya makubaliano ya Ouagadougou yaliyowezesha kufanyika kwa uchaguzi wa Rais.

 (SAUTI YA BAN KI-MOON 1)

 Mkutano wa viongozi hao umefuatiwa na ule wa mawaziri ambapo Ban ulioandaliwa na serikali yaMali. Ban amekaribisha mkutano huo na kusema ni fursa ya kusikiliza tashwishwi na vipaumbele vya nchi za eneo hilo.

 (SAUTI BAN KI-MOON )