Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujiamini na kuchukua hatua stahili mapema siri ya mafanikio: Samson Gachia

Kujiamini na kuchukua hatua stahili mapema siri ya mafanikio: Samson Gachia

Hatimaye maonyesho ya wiki moja ya miradi bunifu isiyo na madhara kwa mazingifa yamefikia ukingoni  hukoNairobiKenyaambapo imeelezwa kuwa miradi yenye thamani ya dola Miliono 450 za kimarekani imewekewa ahadi kati ya wawekezaji na serikali, vikundi mbali mbali, miradi ambayo ikitekelezwa italeta fursa ya ajira, itainua uchumi huku ikijali mazingira. Maonyesho hayo yalishuhudia utoaji tuzo kwa washiriki katika makundi mbali mbali ikiwemo ubia kwa maendeleo. Miongoni mwao ni Samson Gachia anayeongoza kampuni ya Cobitech Biogas mjiniNairobi. Mwenzetu Jason Nyakundi alipata fursa ya kuzungumza naye kuelezea kile alichoshinda na matarajio yake. Hapa anaanza kwa kuelezea kule alikoanzia.