Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera za uchimbaji madini zimeengua wanawake: Waziri Simba

Sera za uchimbaji madini zimeengua wanawake: Waziri Simba

Mkutano wa siku mbili wa ngazi ya mawaziri ulioangalia suala la jinsia kwenye sekta ya madini umemalizikaTanzania. Shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake, UN-Women liliandaa mkutano huo kwa ushirika na Publish What You Pay.

Washiriki walikubaliana kuwa wakati umefika wanawake washiriki kwa kina kwenye sekta hiyo. Miongoni mwao ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania, Sophia Simba ambaye Stephanie Raison, Afisa Habari wa UN-Women Dar es salaam alipanga mahojiano naye yanayofanywa hapa Studioni na Assumpta Massoi. Kwanza Waziri Simba anaelezea athari za uchimbaji madini kwa wanawake.

(Mahojiano)