Wanafunzi wakimbizi wa kipalestina warejea shule na matumaini

4 Oktoba 2013

Huko Lebanon hii leo mwaka mpya wa masomo umeanza vyema kwa watoto wakimbizi wa kipalestina wanaoishi nchini humo pamoja na wale waliolazimika kukimbilia Lebanona kutokana na machafukoSyria. Hali hiyo inatokana na msaada wa vifaa vya muhimu vya shule viliyotolewa kwa pamoja na umoja wa Ulaya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na shirika la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA. Wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo kwenye shule ya wasichana ya maandalizi huko Nablus, Lebanon, Mkuu wa kitengo cha maendeleo endelevu kutoka EU Marcello Mori amesisitiza umuhimu wa elimu na mpango wa UNRWA akiongeza kuwa hivi karibuni Umoja wa Ulaya umekubali kuipatia UNRWA Euro Milioni Sita kwa ajili ya kuwapatia elimu watoto Elfu Sita  kwa miaka miwili.