Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa ILO waangazia faida za kuajiri watu wenye ulemavu

Mkutano wa ILO waangazia faida za kuajiri watu wenye ulemavu

Wawakilishi kutoka shirika la kazi duniani, ILO na kampuni za kimataifa zaidi ya 20 wanakutana huko Shanghai, China kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya manufaa ya kuajiri watu wenye ulemavu. George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Wakati wa mkutano huo washiriki walidhihirisha kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kujumuishwa kwa mafanikio makubwa kwenye nguvu kazi kwa kuzingatia mahitaji yao. Niklas Meintrup mmoja wa waandaji wa mkutano huo kwa kushirikiana na ILO amesema kwao wao kutofautiana na kujumuishana ni moja ya misingi wanayozingatia. Amesema kundi hilo ni muhimu sana kwa mafanikio ya biashara zao na hivyo wanaweka mazingira ya kuwaajiri na kuwa nao kwa muda mrefu. Mshiriki mwingine alisema kampuni nyingi sasa zinatambua umuhimu wa kuajiri kundi hilo ambalo idadi yake ni takribani Bilioni Moja duniani kote. Hata hivyo ILO inasema wanapoenda kuomba kazi hukumbwa na vikwazo ikiwemo mazingira yasiyo rafiki.