Skip to main content

Ujumbe wa UNAMI washuhudia hali halisi kambi ya Ashraf

Ujumbe wa UNAMI washuhudia hali halisi kambi ya Ashraf

Ziara ya ujumbe wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI kwenye kambi ya Ashraf iliyokumbwa na mauaji mwishoni mwa wiki, imewezesha kupata picha halisi ya kile kilichotokea na hatimaye wakazi wa eneohilokuruhusu maiti zilizokuwa zimehifadhiwa eneohilokwa muda kusafirishwa hadi Baquba. Ujumbe huo uliongozwa na naibu mwakilishi maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Gyorgy Busztin ambapo walipata fursa ya kuzungumza na wahanga wa tukio hilo na kamanda wa polisi. Mathalani waliona maiti Hamsini na Wawili ambao miiliyaoinaonyesha walipata majeraha ya risasi hususan kwenye kichwa na baadhiyaomikono ikiwa imefungwa kwa kamba. Halikadhalika walishuhudia majengo yaliyoharibiwa na kiasi kadhaa cha vilipukaji huku wakazi wa kambi hiyo wakisema kuwa watu saba mpaka sasa hawajulikani waliko. Akizungumza baada ya ziara hiyo Busztin amerejelea kushutumu kitendo hicho na kutambua taarifa ya serikali yaIraqya kuwasaka wahusika na kuimarisha usalama kwenye kambi.