Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya ukatili wa kingono na kijinsia vyashamiri Somalia: UM

Vitendo vya ukatili wa kingono na kijinsia vyashamiri Somalia: UM

Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa OCHA imesema matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono nchini Somalia umeshamiri na kwamba katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu kumekuwepo na visa 800 vya aina hiyo kwenye mji mkuuMogadishu. George Njogopa na maelezo zaidi(Taarifa ya George)

OCHA inasema kuwa wakati wanawake na watoto wakiendelea kutaabika kwa kukosa makazi,pembezoni wanakabiliwa na kitisho kingine cha kukumbwa na matukio ya kubakwa vitendo vinavyofanywa makundi ya askari wasiojulikana ambao huvalia sare za kijeshi. Matukio mengine ya unyanysaji wa kijinsia wanaokutana nayo wanawake waSomalia ni pamoja na unyanyasaji wa majumbani, kulazimishwa kushiriki kwenye tamaduni zilizopitwa na wakati ikiweo kupatiwa tohara na kulazimishwa kuolewa. Marixie Mercado kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF anasema kuwa, theluthi moja ya wale wanaokumbwa na matukio ya kunyanyaswa kingoni nchini Somalia ni watoto

(Sauti ya Marixie)

“Katika mwaka 2012 UNICEF iliwapa msaada zaidi ya waathirika 2,2000 wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya Kusin na Kati ya Somalia.Kuna huduma za kiafya ambazo hutolewa kwa wakati kwa ajili ya wanawake na wasiachana walioshambuliwa. Pia kuna misaada mingine ya kiungwana.Wasichana na wanawake ndiyo walioko kwenye hatari kubwa ya kukubwa na matukio hayo hasa wanapojihusisha na kazi ya ukusanyaji wa kuni.Kwa hivyo kupitia msaada uliotolewa na serikali ya Japan tumefanikiwa kuwasaidia maelfu ya wanawake na wasichana msaada wa stovu ya kupikia ikiwa ni sehemu ya msaada unaotolewa”