Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya vijana kila Agost 12 mwaka huu inawalenga wafanyakazi wahamiaji:IOM

Siku ya kimataifa ya vijana kila Agost 12 mwaka huu inawalenga wafanyakazi wahamiaji:IOM

Idadi kubwa ya vijana duniani huondoka katika nchi zao za asili na kwenda uhamishoni kwa ajili ya kusaka ajira na elimu bora.  Ilikuwawezesha vijana hao kufanikiwa kwenye ndoto zao, shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM linaadhimisha siku ya kimataifa ya vijana kwa kauli mbiu isemayo “ Uhamiaji kwa vijana:kuelekea kwenye maendeleo. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE)

Msemaji wa shirika la kimataifa linalohusika na wahamiaji IOM Jumbe Jumbe, anasema kuwa kuwawezesha vijana ili kutimiza ndoto zao za mafanikio ni jambo muhimu ambalo linawawezesha wafika salama katika nchi wanazokwenda.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

IOM inasema kuwa idadi ya wahamiaji vijana wanasafiri nchi za ng’ambo kwa kufuata taratibu halali na zile za chini kwa chini imeongezeka .Kulingana na Jumbe, vijana hao wanaweza kuchukua uamuzi wa busara kwa kutojiingiza kwenye uhamiaji haramu, iwapo vijana hao watapatiwa taarifa za kutosha.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

 IOM kwa sasa inaendelea kushirikiana na shule pamoja na vyuo vikuu ili kutoa elimu juu ya uhamiaji kwa vijana