Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu ataja madhila yanayokumba wahamiaji vijana

Katibu Mkuu ataja madhila yanayokumba wahamiaji vijana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake kwa siku ya kimataifa ya vijana Agosti 12 mwaka huu na kutaja baadhi ya sababu zinazofanywa vijana kuhama nchi zao. Ujumbe wa Bwana Ban umejikita kwenye mada hiyo kwa kuzingatia maudhui ya mwaka huu kwa siku hiyo ambayo ni Vijana na uhamiaji.

(SAUTI YA BAN)

“Vijana wanahama kwa sababu nyingi. Baadhi yao wanakimbia mateso, wengine wanakimbia matatizo ya kiuchumi. Baadhi wanaondoka peke yao, wengine na familia zao kama  wazazi, ndugu, na hata watoto wao wenyewe. Kuna  wale  ambao wanaenda kuungana na jamii lakini wengine ni lazima waanze upya. Wakiwa ni kupitia  tu au wamefika eneo wanapowenda, wengi wa wahamiaji vijana wanakabiliana na changamoto kubwa zikiwemo za ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa aina nyingine na pia ukiukwaji wa haki za binadamu. Wanawake vijana hasa wanakabiliana na hatari ya kubakwa na kunyanyaswa.”

Katibu Mkuu amesema ni vyema kuangazia mchango wa vijana wahamiaji kiuchumi, kitamaduni na kijamii kwa nchi wanazotoka, kule wanakopitia na hata makaziyaoya mwisho. Mathalani fedha wanazotuma kwa familia zao zinasaidia kuboresha maisha.  Ametaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, vikundi vya vijana na serikali kushirikiana kuendeleza haki za vijana kwa mustakhbali stahili wa dunia.