Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bi Robinson asisitiza msimamo wake kuhusu amani DRC

Bi Robinson asisitiza msimamo wake kuhusu amani DRC

Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa UM kwenye nchi za Maziwa Makuu, Mary Robinson, amesema anaunga mkono kwa dhati azimio namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Bi Robinson amesema kuwa azimiohiloni la wazi na linatoa nafasi nzuri ya kimataifa kuhakikisha amani na usalama wa DRC. Robinson amesema hayo akizungumza na Radio Okapi ya Umoja wa Mataifa DRC, baada ya madai ya vyombo vya habari nchini humo kwamba anataka kubadilisha azimiohiloili kupunguza majukumu ya brigedi ya kimataifa, na badala yake kuyapa kipaumbele majadiliano ya kisiasa kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23. Bi Robinson amekana madai hayo na kufananua msamimo wake akisema:

 Kweli kuna wale ambao wanachukua msimamo wangu kwa makosa na ningependa  kufafanua na kuurudisha katika dhana yake. Ninarudia tena msimamo wangu unaounga mkono kabisa azimio 2098 na mapendekezo yake yote, na pia naunga  mkono MONUSCO. Nia yangu ni kufanya kazi kwa  karibu na Mwakilishi maalum mpya Martin Kobler, ili kusaidia juhudu za MONUSCO. Tayari tuna uhusiano mzuri  sana. Malengo yetu sote ni yale yale. Tutachukua hatua kwa pamoja na kuungana mkono ili kusaidia serikali na watu wa DRC katika harakati ya kupata amani.  

 Bi Robinson amesema Brigedi ya kimataifa tayari imefika nchini na inachukua hatua kwa utaratibu ikishirikiana na serikali ya DRC ili kukabiliana na hali ilivyo nchi.