Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa msaada zaidi kwa wakimbizi wa Syria

IOM yatoa msaada zaidi kwa wakimbizi wa Syria

Shirika la la kimataifa la uhamiaji IOM limeendelea kutoa msaada kwa wakimbizi wa Syria ambapo hivi sasa linawasaidia wakimbizi wa ndani takribani elfu tano huko mashariki mwa nchi hiyo katika jimbo la Lattakia ambao waliwasili Agosti 5 kufuatia kushamiri kwa mapigano. Wakimbizi hao wengi wao ni watoto, wanawake na wazee na wengi wao huwasili hapo wakiwa taabani. Msemaji wa IOM Jumbe Omari jumbe anafafanua zaidi.

 (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)