Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlo wa mchana shuleni uliotolewa na WFP umebadili maisha yangu: Peter

Mlo wa mchana shuleni uliotolewa na WFP umebadili maisha yangu: Peter

Mpango wa utoaji wa mlo wa mchana shuleni umekuwa ukitekelezwa katika nchi mbali mbali duniani, miongoni mwa nchi hizo ni Kenya ambapo imeelezwa kuwa utoaji mlo wa mchana shuleni umesababisha watoto siyo tu kupenda kwenda shule bali pia umewezesha kuongeza uelewa katika masomo. Miongoni mwa wanufaika wa mpango huo ni Peter Mumo ambaye katika makala hii ya wiki iliyoandaliwa na Jason Nyakundi kutoka Nairobi Kenya anatueleza vile ambavyo mlo wa mchana uliovyokuwa na nafasi kubwa katika kumwezesha kuwa na maisha bora hivi sasa.