Tukikabiliana na migogoro tutakuza amani na maendeleo:Ban
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumza katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya urafiki na kusema ni muhimu kukabiliana na hali za kutoelewana ambazo zinasababisha mivutano na migogoro katika dunia ya leo.Katika ujumbe wake kwa siku hiyo Bwana Ban amekumbusha kwamba mshikamano wa kibinadamu ni muhimu katika kukuza amani ya kudumu na maendeleo endelevu.
Amesema siku hii itumike kukuza mahusiano ambayo yanaimarisha ubinadamu wa pamoja na kukuza ustawi wa familia ya binadamu.