Misaada ya UNICEF haifikii familia za vijijini huko Damascus

Misaada ya UNICEF haifikii familia za vijijini huko Damascus

Takribani raia Milioni Moja nukta Mbili wa Syriawanaoishi maeneo ya vijijini mashariki mwa mji mkuu waSyria,Damascusbado wana mahitaji makubwa ya kibinadamu, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF. Yaelezwa ya kwamba misafara ya Umoja wa Mataifa ikielekea maeneo hayo ikiwa na misaada kwa familia Elfu Tano imekwama kwa miezi kadhaa sasa kutokana na mapigano yanayoendelea. Kwingineko nchini humo hata hivyo UNICEF imesema imeweza kusambaza vifaa ikiwemo vile vya chanjo huko Alepppo na vifaa vya shule kwa wanafunzi elfu Sabini.  Huko Al Qusayr, licha ya mapigano makali, UNICEF imeweza kukarabati jenereta kwenye pampu ya maji inayohudumia watu Milinoi Moja nukta Tanu. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

 

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

 

“Mwezi huu UNICEF inasambaza sabuni kwa watu Milioni Kumi nchini kote. Zaidi ya kaya Laki sita ambako usalama wa maji  ya kunywa ni wa mashaka , wao watapata vidonge vya kutakatisha maji. Vifaa vya usafi binafsi na vya kutupia taka vitafikia watu Milioni Mbili. Kwa pamoja na wahudumu wa kujitolea wa wizara ya afya na taasisi ya Hilal nyekundu tumwafikia watoto zaidi ya Milioni Moja kwa ajili ya chanjo dhidi ya surua na wengi wao wako kwenye ukanda wa vita.