UNICEF, WHO waonya kuhusu hali mbaya ya usafi duniani

13 Mei 2013

Ripoti ya pamoja ya mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la la afya, WHO na shirika la kuhudumia watoto UNICEF inaonyesha kwamba theluthi moja ya idadi ya watu duniani itaendelea kutokuwa na usafi hadi mwaka 2015.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la taarifa ya maendeleao ya usafi na unywajji wa maji ,2013, inahadharisha kuwa kwa kasi ya sasa ya ufikiwaji wa lengo la maendeleo ya milenia la kupunguza kwa asilimia hamisini idadi ya watu ambao mwaka 1990 walikuwa wanaishi bila usafi litakwama kwa asilimia 8 ambao ni sawa na nusu bilioni ya watu.

Mkurugenzi wa afya aya jamii na mazingira wa WHO Dr Maria Neira anasema kuna haja ya dharura ya kuhakikisha dhamira ya kisiasa na fedha, ili dunia ipige hatua katika kufikia lengo hili la usafi la maendeleoa ya milenia

Ripoti hiyo kadhalika imetoa wito wa dharura kwa Makamu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Elaisson kujumuisha nguvu ili kukomesha swala la kujisaidia hadharani kufikia mwaka 2025.

Kwa upande wake Mkuu wa usafi wa maji wa UNICEF Sanjay Wijesekera amesema hali hii ni dharura inayotisha kuliko tetemeko kuu au Tsunami ambapo kila mwaka mamia ya watoto hufa kutokana na kutokuwa na usafi ikiwamo maji safi na salama na kutaka kutafutiwa ufumbuzi kwa kile alichokiita janga la kibinadamu.