Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simu za viganjani kuboresha elimu ya msingi Nigeria

Simu za viganjani kuboresha elimu ya msingi Nigeria

Shirika la Umoja  wa Mataifa la la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO linashirikiana na wadau wake kuboresha elimu ya msingi nchini Nigeria kupitia teknolojia ya simu ya kiganjani.  Mratibu wa mradi huo kutoka UNESCO Steven Vosloo amesema kupitia simu za viganjani ambazo kwa sasa karibu kila mtu anamiliki nchini humo, walimu watapokea ujumbe wa masomo kila siku pamoja na ushauri wa kielimu kwa ajili ya wanafunzi wao.  Vosloo amesema kwaNigeria, ambayo ni moja ya nchi duniani zenye kiwango cha juu cha wasiojua kusoma na kuandika, teknolojia ya simu inaweza kuwa fursa ya kuboresha elimu katika maeneo ambayo walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu na si rahisi kufikika. Mradi huo utatekelezwa kwa wiki 72 tangu mwalimu mhusika atakapokuwa amejiandika bure na ataweza kupokea maelekezo ambayo pia yanaweza kumuunganisha na vyanzo vingine vya mafunzo.  Mipango ya kuendeleza elimu kupitia simu za kiganjani tayari inatekelezwaMsumbiji,Kenya, Afrika Kusini naNigerna kutoa fursa hata kwa wanawake na watoto wa kike kupata elimu.