Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na benki za kikanda wajadili jinsi ya kuchochea kasi ya maendeleo ya milenia

UM na benki za kikanda wajadili jinsi ya kuchochea kasi ya maendeleo ya milenia

Mikutano ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon huko Washington D.C imemkutanisha na marais wa benki za kikanda duniani akiwemo wa Benki ya maendeleo ya Afrika Donald Kaberuka na wa benki ya ukarabati na maendeleo ya Ulaya Suma Chakrabati ambapo wamezungumza vile ambavyo pande mbili hizo zitachochea kasi ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia wakati huu ambapo zimebakia siku chini ya Elfu Moja. Viongozi hao mathalani wamejadili nyaraka ya makubaliano kati benki za maendeleo za kikanda na Umoja wa Mataifa juu ya kuboreshwa takwimu kwa maendeleo endelevu. Bwana Ban amesema nyaraka hiyo inachochea ushirikiano kwa maslahi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wakati huu ambapo dunia imefikia kipindi muhimu cha maandalizi ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 Disemba, kipindi ambacho ni ukomo wa malengo ya milenia.