Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UM aelezea masuala muhimu kwa mwaka 2011

Mkuu wa UM aelezea masuala muhimu kwa mwaka 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kwa mwaka huu ameainisha masuala muhimu kwa 2011.

Masuala hayo ni pamoja na kuchagiza maendeleo endelevu, mbadiliko ya hali ya hewa, kuwawezesha wanawake, masuala ya kuhakikisha nyuklia yaiishii mikononi mwa magaidi, kutatua migogoro na kuhakikisha dunia inakuwa mahapa salama pa kuishi.

Ameziambia nchi 192 wanachama wa Umoja wa Mataigfa kwamba mafanikio ya masuala manane anayoyapa kipaumbele kwa mwaka huu ujao yatategemea sana ushiriki wao. Ban akizungumza na waandishi wa habari ameonya kwama mwaka 2010 ulikuwa wa changamoto kubwa kwa Umoja wa Mataifa basi 2011 utakuwa zaidi.

Ban ameyataja masuala hayo manane kama kwanza maendeleo endelevu yanayojumuisha wote, pili

Kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, tatu kutoa fursa zaidi za kuwawezesha wanawake, nne kudumisha amani na kuifanya dunia kuwa mahali pema na salama pa kuishi.

Tano Ban kudumisha haki za binadamu, sita kushughulikia migogoro na jinsi ya kukabili majanga hasa akitolea funzo lililopatikana Haiti. Saba kuongeza juhudi za kupokonya silaha hasa za nyuklia na mwisho kudumisha na kuboresha Umoja wa Mataifa kuanzia ndani.

Pia amerejea wito wake wa kumtaka Laurent Gbagbo Rais aliyeshindwa uchaguzi Ivory Coast kuachia madaraka na kuleta amani nchini humo.