Maji yasiyo safi na salama yaua watoto kila siku: UNICEF

22 Machi 2013

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya maji hii leo, Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limezishauri  serikali, mashirika ya umma na wananchi wa kawaida kutambua kuwa takwimu zozote zinazotolewa, zinajumuisha pia watoto. Mkuu wa kitengo cha maji na usafi ndani ya UNICEF Sanjay Wijesekera, amesema kuna wakati ambapo msisitizo unawekwa kwenye takwimu kubwa na hivyo kushinwda kuona majanga ya kibinadamu yanayosababishwa na kila takwimu akigusia athari za maji machafu kwa uhai wa watoto. Jason Nyakundi na ufafanuzi zaidi.

(SAUTI YA JASON)

Kote duniani takriban watoto 2000 walio chini ya miaka mitano wanakufa kila siku kutokana na magonjwa ya kuhara huku kati ya vifo 1800 vikiwa vinahusiana na maji na usafi. UNICEF inasema kuwa iwapo mabasi 90 yaliyojaa watoto wadogo wanaoanza masomo yatahusika kwenye ajali kila siku bila ya kuwepo manusura ulimwngu utachukua tahadhari. UNICEF inaendelea na kusema kuwa hili ndilo hufanyika kila siku  kutokana na maji machafu na kutokuwepo na usafi. Takwimu za UNICEF  kuhusu vifo vya watoto zinaonyesha kuwa nusu ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano hutokea kwenye nchi tano tu zikiwemo India , Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo , Pakistan na China. Wijesekera hataua zilizopigwa tangu mwaka wa tisini zinazonyesha kuwa kuwekeza na kuwa na malengo ya kuafikiwa  kila motto anahitaji kupata maji safi ya kunywa na usafi wakati huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud