Skip to main content

UNDP yapokea ripoti ya awali ya maendeleo baada ya 2015

UNDP yapokea ripoti ya awali ya maendeleo baada ya 2015

Shirika la Mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, leo limepokea ripoti ya utafiti wa awali kuhusu maoni ya watu mbalimbali juu ya mkakati wa maendeleo baada ya Mpango wa Maendeleo ya Millenia mwaka 2015.

Ripoti hiyo iliyochukuliwa katika picha na kupewa jina ‘‘Majadiliano ulimwenguni yaanza”  imehusisha wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 100 duniani ambapo vipaumbele vinavyotarajiwa kuchukua nafasi ni Malengo ya Maendeleo ya Milenia kuendelezwa kulingana na kukua kwa tofauti baina ya nchi na madhara ya utandawazi, changamoto za uharibifu wa mazingira, ajira na ghasia pamoja na ushirikishwaji na kusimamia mikakati ya maendeleo baada ya 2015.

 Katika mpango huo wa kukusanya maoni juu ya mikakati ya maendeleo baada ya 2015, Umoja wa Mataifa umehusisha watu laki mbili kutoka nchi 189 wanaotoa maoni yao kupitia vyombo vya habari, simu za viganjani, makongamano, pamoja na kura, ambapo UNDP imesisitiza kuwa makundi maalum kama walemavu, wanawake,vijana na wazawa wanashirikishwa katika mpango huo.