Waliokimbia makazi yao Mali wataka kurejea nyumbani: IOM

15 Februari 2013

Utafiti uliofanywa na  Shirika la Uhamiaji Duniani (IOM) unaonyesha kuwa asilimia 93 ya jamii zilizotimuliwa kutoka maeneo ya kaskazini mwa Mali na ambazo sasa zinaishi katika mji mkuu Bamako na mji jirani Koulikoro zinataka  kurejea nyumbani mara tu hali ya usalama na ya kiuchumi itapoimarika.

Utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu mapema mwezi huu ulihusisha familia 836 kutoka miji ya kaskazini ya Timbuktu na Gao, ambayo ilikuwa chini ya uvamizi wa waasi hadi kuokolewa na vikosi vya Ufaransa na Mali mwezi Januari.

Halikadhalika utafiti huo unayonyesha asilimia 93 ya watu waliohojiwa wanakusudia kurudi katika maeno waliotoka. Asilimia 23 wanakusudia kurejea mwezi huu wakati asilimia 32 wamesema watareja kati ya mwezi machi na mwisho wa mwaka huu.  Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM:

(SAUTI YA JUMBE

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter