Uzalishaji wa mazao ya misitu bado ni wa kusuasua tangu kutokea anguko la uchumi wa dunia

Uzalishaji wa mazao ya misitu bado ni wa kusuasua tangu kutokea anguko la uchumi wa dunia

Uzalishaji wa mazao yatokanayo na misitu unaarifiwa kusuasua tangu kushuhudiwa kwa mkwamo wa uchumi wa dunia, huku mataifa yaliyoko katika kanda ya Asia-Pacific ndiyo yakishika nafasi ya kwanza.

Hata hivyo China ndiyo iliyotajwa kuwa ndiyo inayofanya vizuri zaidi ikilinganishwa na mataifa mengine duniani.

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo duniani FAO inasema kuwa kiwango cha uzalishaji mazao ya misitu kilikuwa kwa wastani wa asilimia 4 katika kipindi cha mwaka 2011.

Ripoti inafungamanisha hatua ya kukuwa kwa kiwango kidogo cha mazao hayo na tukio la kuanguka kwa uchumi wa duniani kulikojitokeza katika miaka ya hivi karibuni.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kiwango cha uzalishaji siyo cha kuridhisha na kubainisha takwimu ambazo zinatoa ulinganifu unaopishana katika kipindi cha mwaka 2011 na 2010.