Ban na Brahimi wasisitiza mapigano Syria yasitishwe sikukuu ya Eid El-Haji

19 Oktoba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, BanKi-Moon na mwakilishi maalum wa UM wa muungano  wa nchi za Kiarabu wameziomba pande zote husika katika mgogoro wa Syria kusikia wito uliotolewa kutakiwa kusitisha mapigano wakati wa kipindi cha sikukuu ya Eid El Haji ili kutoa fursa kwa raia wa nchi hiyo kusherehehea siku hiyo takatifu kwa amani na utulivu.

Ban na Brahimi wametoa taarifay ya pamoja wakiirejelea wito wa awali uliotolewa na Brahimi ambaye pia ni Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mgogoro wa Syria.

Makatibu hao wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu, wamesema iwapo wito huo utaitikiwa, itakuwa ni fursa kwa mchakato wa amani wa kisiasa ambao utakidhi matarajio ya wananchi wa Syria ya kuwa na demokrasia, usawa na haki.

Wameongeza kuwa kadri mgogoro huo unavyokua, itakuwa vigumu zaidi kuupatia suluhisho la kisiasa na kuijenga nchi hiyo na kutaka Syria, pande za kikanda na kimataifa kuchukua hatua stahiki kufanikisha jitihada za Brahimi za kuleta amani.

Mathalani waimeiomba serikali ya Syria ambayo ni upande wenye nguvu zaidi katika mvutano huo kuonyesha busara na dira ya kusitisha mauaji ya raia na uharibifu ili masuala yote hata kama ni magumu kiasi gain yanaweza kushughulikiwa kwa amani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter