Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama liunge mkono mapendekezo ya Umoja wa nchi za Kiarabu:Clinton

Baraza la Usalama liunge mkono mapendekezo ya Umoja wa nchi za Kiarabu:Clinton

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton amesema wote wana uchaguzi wa kusimama pamoja na watu wa Syria na eneo zima la Mashariki ya Kati au kufanya makosa ya kuruhusu ghasia kuendelea.

Akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la Usalama kuhusu pendekezo la mswaada wa azimio dhidi ya Syria Jumanne jioni Bi Clinton amesema katika wiki za karibuni serikali ya Syria imezidisha mashambulizi kwa raia na hata kusababisha Umoja wa nchi za Kiarabu kusitisha mpango wake nchini humo.

Amesema umewadia wakati kwa Baraza la Usalama kusikiliza matakwa ya watu wa Syria kwa kuunga mkono mapendekezo ya Umoja wa n chi za Kiarabu yanayotaka serikali ya Syria kusitisha mara moja mashambulizi dhidi ya raia na kuwahakikishia uhuru wa kuandamana.

Pia Syria lazima iwaachilie mahabusu wote, iwarejeshe wanajeshi makambini, iruhusu waangalizi, wafanyakazi wa misaada na waandishi wa habari.Ameongeza kuwa Marekani iko tayari kushirikiana na wajumbe wa baraza kuunga mkono mtazamo wa Umoja wa nchi za Kiarabu.

(SAUTI YA HILARY CLINTON)

Naye balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa Bashar Al-Jafar amesema inapinga uingiliwaji wowote kutoka nje.

(SAUTI YA BASHAR AL JAFAR)