Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili harakati za amani Mashariki ya Kati

Baraza la Usalama lajadili harakati za amani Mashariki ya Kati

Mratibu maalumu wa UM kuhusu Mashariki ya Kati, Robert Serry, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika ripoti yake kuwa hali ya mvutano baina ya Israeli na Palestina bado imesalia kuwepo, licha ya kwamba vitendo ambavyo vinaleta kutokuaminiana vimepungua.  Amesema mathalan katika kipindi ambacho ripoti hiyo ilikuwa inaandaliwa, hakukuwepo na tangazo la ujenzi wa makazi mapya ya walowezi, mashambulizi ya Israeli huko Ukingio wa Magharibi yalipungua, na kwamba majengo matatu ya makazi yalibomolewa tarehe 18 mwezi huu.  Amesema anaunga mkono ziara ya Rais wa Marekani ya kujaribu kuendeleza mchakato wa amani, na kutaka mazingira chanya yaendelee kuwepo ili mchakato wa amani uendelee kuchukuwa mkondo wake.