Ban ahimiza Kustahimiliana na Amani wakati wa Michezo ya Olimpiki London

27 Julai 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameutaka ulimwengu kudumisha amani wakati wa michezo ya Olimpiki ambayo imeanza mjini London, Uingereza.

Bwana Ban ambaye ameshangiliwa na umati mkubwa watu wakati akiubeba mwenge wa Olimpiki katika mitaa ya London siku ya alhamis, alikuwa amewasili London moja kwa moja kutoka Bosnia na Herzegovina, ambako alizuru mji wa Srebrenica, ambako zaidi ya watu 7, 000, wanaume na wavulana wa Kiislamu waliuawa mwezi Julai 1995, wakati wa vita vya kanda ya Balkan.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa walikuwa miongoni mwa watu zaidi ya 8, 000 walioubeba mwenge wa Olimpiki, tokea taifa la Ugiriki, asili ya mashindano ya Olimpiki, hadi London katika kipindi cha siku 70 zilizopita.

Bianca Kopp kutoka Austria, alinusurika shambulizi la kigaidi mwezi Agosti 2011, kwenye jingo la Umoja wa Mataifa mjini Abuja, Nigeria, naye Julius Mwelu, aliliwakilisha shirika la makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat, lenye makao yake nchini Kenya anakotoka.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter