Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji kukabiliwa na gharama kubwa kuhifadhi taka

Miji kukabiliwa na gharama kubwa kuhifadhi taka

Ripoti mpya iliyotolewa na Bank ya dunia inasema kuna asilimia 70 ya ongezeko la taka ngumu mijini.

Ripoti hiyo ambayo inaelezea hali ya taka duniani inakadiria kwamba kiwango cha taka zinazokusanywa katika makazi ya watu mijini kati ya sasa na mwaka 2025 kitaongezeka kutoka tani bilioni 1.3 kwa mwaka na kufikia tani bilioni 2.2 kwa mwaka huku kiwango kikubwa cha taka hizo kikipatikana katika miji inayokuwa kwa kasi ya nchi zinazoendelea.

Gharama ya kudhibiti taka hizo kwa mwaka Bank ya dunia inakadiria zitaongezeka kutoka dola bilioni 250 hadi kufikia dola bilioni 375 na nchi zitakazoumia zaidi ni zile za kipato cha chini.

Ripoti hiyo iitwayo “What a waste: mtazamo wa kimataifa wa kudhibiti taka ngumu, kwa mara ya kwanza inatoa takwimu za jinsi ya kutengeneza taka hizo, kukusanya, kuzihifadhi na kuzitupa kwa kila nchi na kila kanda. Dan Hoornweg ni mtaalamu wa masuala ya miji katika Bank ya dunia.

(SAUTI YA DAN HOORNWEG)