Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UM wajadili njia bora za ufikishaji taarifa za kijographia kwa maendeleo

Mkutano wa UM wajadili njia bora za ufikishaji taarifa za kijographia kwa maendeleo

Wawakilishi kutoka nchi 90 na wajumbe kutoka mashirika mbalimbali na jumuiya za kiraia wanakutana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Korea leo kwa ajili ya mikutano kadhaa ya Umoja wa mataifa. Mikutano hiyo inajikita katika kuboresha teknolojia ya udhibiti wa ukusanyaji, utunzaji, uendeshaji na ufikishaji taarifa za kijografia au geospatio na kuzitumia taarifa hizo kukabiliana na changamoto za kijamii na kichumi zinazoikabili dunia hivi sasa.

Sha Zukang mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kiuchumi na kijamii anasema katika muongo mmoja uliopita teknolojia mpya imebadilisha kabisa upatikanaji wa taarifa za geospatioal na umuhimu wa kuzitumia taarifa hizo. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)