Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua wavuti kusaidia nchi kutekeleza miradi ya mazingira

UM wazindua wavuti kusaidia nchi kutekeleza miradi ya mazingira

Umoja wa Mataifa umezindua wa wavuti yaani website ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kuwa na njia ya kupata fedha kwa ajili ya kufadhilia miradi inayolenga mazingira.

Nchi hizo kwa hivi sasa zinahitaji si chini ya dola bilioni 100 kwa mwaka ili kurekebisha mifumo yake kufuatana na mabadiliko ya tabia nchi na kiasi kingine cha dola milioni 175, kufikia shabaya iliyowekwa ya mwaka 2030.

Mkurugenzi wa Benki ya dunia katika kitengo cha mazingira anayehudhuria mkutano wa mazingira huko Cancun, Mexico Warren Evans amesema kuwa wavuti hiyo ni hatua itayosaidia kutoa fursa ya wapi kunaweza kupatikana vyanzo vya fedha.

Ameeleza kuwa nchi nyingi zinazoendelea hazina vyanzo vya habari vya kutosha kujua wapi kunaweza kupatikana fedha za kwa ajili ya kufadhilia miradi ya mazingira.