UM umezindua mipango ya kuchagiza nishati kwa wote

21 Septemba 2011

Kushindwa kumudu nishati safi na ya gharama nafuu kunatishia kufikia malengo ya kimataifa ya kutokomeza umasikini na magonjwa, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyezindua mipango mipya ya kuhakikisha nishati inapatikana kwa wote duniani.

Katika ujumbe wake uliowasilishwa na Naibu Katibu Mkuu Asha Rose-Migiro Ban amesema nishati ni muhimu kwa maendeleo ya binadamu, katika afya, elimu, ajira na uchumi na ametangaza kuundwa kwa jopo la ngazi ya juu kuhakikisha nishati endelevu kwa wote. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter