Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huenda idadi ya wakimbizi wanaohitaji makao ikaongezeka: UNHCR

Huenda idadi ya wakimbizi wanaohitaji makao ikaongezeka: UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa idadi ya wakimbizi ambao wanahitaji kupelekwa nchi zingine huenda ikapanda na kufikia wakimbizi 780,000 kwa muda wa miaka mitatu ijayo. UNHCR inasema kuwa huenda idadi kubwa ya wakimbizi wakasalia kwenye matatizo ikiwa nchi hazitaongeza idadi ya wakimbizi zinazoweza kuwapa hifadhi.

Mwaka 2010 UNHCR iliwasilisha majina ya wakimbizi 108,000 waliostahili kupata makao lakini hata hivyo ni wakimbizi 73,000 waliofanikiwa kupewa makao nchi zingine. Nchi 25 kwa sasa zinawapa makao wakimbizi huku Marekani ikiongoza kwa kuwapa wakimbizi wengi zaidi makao. Wei Meng Lim Kabaa ni mkuu wa shughuli za kutoa makao kwenye shirika la UNHCR

(SAUTI YA WEI MENG LIM KABAA)