Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka kuwepo matumizi na nishati safi

UM wataka kuwepo matumizi na nishati safi

Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuwepo kwa mabadiliko kwenye mifumo inayotumika katika uzalishaji wa kawi na chakula kama moja ya njia ya kumaliza umaskini na kuzuia hatari iliyopo kunapoendelea kushuhudiwa mabadiliko ya hali ya hewa. Kulingana na ripoti yake ya kila mwaka Umoja wa Mataifa unasema kuwa kuna haja ya kuwekeza kwenye teknolojia za nishati safi

Akizundua ripoti mjini Geneva Naibu Katibu kwenye idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kiuchumi na kijamii Sha Zukang amesema kwa idadi ya watu duniani inatarajiwa kuongezeka kwa watu milioni mbili itimiapo mwaka 2050.

(SAUTI YA SHA ZUKANG)

Ripoti hiyo pia inasema kwa takriban dola trilioni 1.9 zitahitajika kila mwaka katika kuwekeza kwenye teknolojia safi nusu yake ikienda kwenye nchi zinazoendelea.