Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yafanikisha kilimo cha umwagiliaji Sudan

UNDP yafanikisha kilimo cha umwagiliaji Sudan

Jumla ya wakulima 1,000 walioko Kaskazini mashariki wa Sudan wamefaidika na mpango ulioratibiwa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na maendeleo UNDP ambalo liliwasambazia wakulima hao vifaa vya kisasa kwa ajili ya kilimo.

Wakulima hao wamefanikiwa kuongeza uzalishaji mali na katika kipindi cha mavuno walifanikiwa kupata mafuno zaidi ambayo yamewafanya kupata tija kubwa kwenye soko.

Shirika hili la umoja wa mataifa liliwasambazia vifaa mbalimbali ikiwemo pump za maji na mashine za kusuma umeme ambazo zimezesha wakulima hao kunondokana na kilimo cha kutegemea mvua pekee.

Wakulima hao wameelezea mafanikio hayo ambayo wamedai kuwa kuwepo kwa mifumo ya kisasa ya ulimaji ikiwemo kuwepo kwa kilimo cha umwagiliaji, kumeleta mapinduzi makubwa kwenye eneo hilo.