Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa vyombo vya habari ni nguzo katika kujenga jamii ya kidemokrasia:UM

Uhuru wa vyombo vya habari ni nguzo katika kujenga jamii ya kidemokrasia:UM

Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari na kauli mbiu mwaka huu ni "vyombo vya habari karne ya 21, mipaka mipya na vikwazo vipya" ikijikita katika ongezeko la jukumu la internet na mtandao mpya wa mawasiliano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema uhuru wa vyombo vya habari ni moja ya nyenzo muhimu katika kutanabaisha makosa na kuijulisha jamii pale serikali zinapokwenda kombo na kujaribu kujikinga na kuumbuliwa.

Ameonya kwamba pamoja na juhudi zote kuna vikwazo vipya dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari vinavyowekwa na serikali ikiwemo kufuatiliwa, kudhalilishwa na kuijulishahujwa kwa habari kwenye tovuti.

Katika siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Mai 3 mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni Irina Bokova amezitaka serikali zote kutimiza wajibu wao wa kulinda na kuchagiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari ambao ndio msingi wa jamii ya kidemokrasia

(SAUTI YA IRINA BOKOVA)

Naye mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesisitiza jukumu linasalia kwa serikali kuhakikisha zinatimiza matakwa ya wananchi wake na hususani kuwapa uhuru wa kujieleza na haki za msingi za binadamu akitolea mfano wa hali inayoendelea Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)