Skip to main content

Machafuko duniani yanatoa changamoto kwa UM:Ban

Machafuko duniani yanatoa changamoto kwa UM:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa hivi sasa unakabiliana na changamoto kubwa kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea duniani.

Akizungumza kwenye taasisi ya uhusiano wa kimataifa ya Kiev nchini Ukraine alikohitimisha ziara yake hii leo Ban amesema machafuko nchini Ivory Coast kwa mfano jumuiya ya kimataifa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa wamekuwa na msimamo mmoja kwamba katika demokrasia watu wana haki ya kuchagua viongozi wao na viongozi ni lazima waheshimu hilo, kwani uongozi unatoka kwa watu.

Amezungumzia pia mchango wa Ukraine kwa helkopta zake kutumika kuharibu silaha nzito zilizokuwa zikitumiwa na Laurent Gbagbo kuuwa raia na kushambuliwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa Ivory Coast.

Na kuhusu hali inayoendelea Afrika ya Kaskazini hususan Misri, Tunisia na Libya Ban amesema ni fursa ya kupata kidemokrasia.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)