Skip to main content

Upatikanaji wa mbegu bora utasaidia kuinua kilimo:FAO

Upatikanaji wa mbegu bora utasaidia kuinua kilimo:FAO

Katika ripoti yake iliyochapishwa leo juu ya mwongozo wa sera, shirika la umoja wa mataifa la chakula la kilimo FAO limeeleza umuhimu wa kuwa na vyanzo vya uhakika na imara vya upatikanaji wa mbegu ili kusaidia kuwa na uhakika wa chakula kwa nchi zinazoendelea.

Takwimu zilizotolewa na benki ya dunia zinaonyesha kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji unaofikia zaidi ya asilimia 50, kutokana wakulima wake kupatiwa huduma bora za mbegu na kwa wakati muuafaka.

Katika miaka ya hivi karibuni serikali ya nchi nyingi zinazoendelea zimekuwa zikipunguza kiwango cha uwekezaji kwenye mbegu kwa matarajio kwamba sekta binafsi zitafidia pengo hilo.Hata hivyo FAO inataka kuwepo kwa msukumo mpya ambao utawawezesha wakulima kupata mbegu bora tena kwa wakati ili kusukuma mbele shughuli za kilimo