Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ametoa ombi la kimataifa kufadhili misaada ya kibinadamu 2011

Ban ametoa ombi la kimataifa kufadhili misaada ya kibinadamu 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kimataifa kufadhili shughuli za misaada ya kibinadamu kwa mwaka huu wa 2011.

Akizungumza mjini Geneva hii leo katika uzinduzi wa ombi hilo 2011 consolidated appeal amesema kwa pamoja sote tunahitaji kuongeza juhudi ili kupata fedha kwa ajili ya msaada wa dharura, na shughuli za kuokoa maisha ya watu.

Amesema kazi ya kupata fedha za msaada isiachwe tuu kuwa ni ya hiyari . Ameoongeza kuwa misaada ya kibinadamu inategemea mchango wa hiyari kutoka kwa nchi wana chama na wahisani binafsi na mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka kila uchao.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa maisha ya watu wengi yanategemea msaada na msaada huo unahitajika zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote. Amesema ingawa kulikuwa na hatua nzuri wakati wa tetemeko la Haiti na mafuriko ya Pakistan lakini maombi mengine ynakwenda polepole na hilo lazima lishughulikiwe mwaka huu 2011. Umoja wa Mataifa umeomba dola bilioni 7.4 kusaidia watu milioni 50 katika nchi 28 duniani.