Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa utalii Afrika umepewa kipaumbele: WTO

Umuhimu wa utalii Afrika umepewa kipaumbele: WTO

Katika mwaka wa pili mfululizo kongamano la uwekezaji katika utalii barani afrika linalofanyika katika maonyesho ya utalii ya kimataifa FITUR 2011 litaongeza muonekano wa afrika kama kituo cha utalii na kuchagiza uwekezaji kama nyenzo ya maendeleo endelevu ya sekta ya utalii.

Kongamano hilo linalofanyika Madrid Hispania linaruhusu wawekezaji kubaini umuhimu na thamani, na msaada wa uwekezaji katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika bara hilo.

Na matokeo ya kuongeza uwekezaji ukuaji wa utalii utakuwa na matunda mazuri barani afrika, hasa uwezo wa kuongeza ajira, pato la nje, kuinua uchumi wa taifa na kuleta maendeleo.

Kongamano hilo linasema faida nyingine kubwa kwa ongezeko la uwekezaji katika sekta ya utalii Afrika ni kusaidia kiuchumi sekta zingine kwa manufaa ya jamii.