Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jua, mvua ni vyetu tukisaka elimu:wakimbizi Tanzania

Picha: UNHCR
Mwanafunzi katika shule ya msingi ya Furaha nchini Tanzania. Picha: UNHCR

Jua, mvua ni vyetu tukisaka elimu:wakimbizi Tanzania

Watoto wakimbizi kwenye kambi tatu nchini Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kupata elimu, maelfu wakilazimika kusomea nje chini ya miti kutokana na ukosefu wa fedha za ujenzi wa madarasa limesema shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR. John Kibego na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JOHN KIBEGO)

Natts …

image
Watoto wakimbizi wa shule ya msingi ya Furaha kambini Nduta mkoani Kigoma nchini Tanzania wakiwa darasani chini ya mti. Mvua ikinyesha inakwamisha elimu. Picha: UNHCR
Watoto wakimbizi wa shule ya msingi ya Furaha kambini Nduta mkoani Kigoma nchini Tanzania wakiwa darasani chini ya mti.

Natts … Hafashimana Euphrasie

Hafashimana Euphrasie mwenye umri wa miaka 14 mkimbizi kutoka Burundi akisema mvua ikinyesha kila kitu kinalowana, iwe upepo mkali, matawi ya miti ya kianguKa na hata jua la kupindukia hawana la kufanya inabidi wavumilie ili wapate elimu. Kwa kumujibu wa UNHCR, ukata wa fedha umesababisha maelfu ya watoto katika kambi za Nduta, Nyarugusu na Mitendeli kusomea nje kutokana na upungufu wa madarasa.  Pamoja na changamoto hizo ni chini ya asilimia 50 ya watoto hao ndio wanaopata elimu ingawa Umoja wa Mataifa unasisitiza elimu ya msingi iwe ni lazima kwa wote. Afisa elimu wa UNHCR kambini hapo ni James Onyango

(CLIP YA JAMES)

“Tunahitaji fedha zaidi, ujenzi wa madara unahitaji fedha zaidi ili kuweka madarasa hapa. Kwa kukosa maneno ninachoweza kusema ni kwamba kinachotokea hapa hakikubaliki.”

image
Watoto wakimbizi wa shule ya msingi ya Furaha kambini Nduta mkoani Kigoma nchini Tanzania wakiwa darasani chini ya mti. Picha: UNHCR
Takwimu za shirika hilo zinaonyesha ni Asilimia tano tu ya wanafunzi hao ndio wanaoweza kupata elimu ya sekondari kama Ndayininahanaze Marie-Gorret

(CLIP YA MARIE-GORET)

UNHCR inasema hali hiyo inawakumba karibu wakimbizi WOTE katika sehemu mbalimbali duniani na waathirika wakubwa ni wale walioko katika nchi za kipato cha chini.

Natts…..