Skip to main content

UM umezindua ombi kuwasaidia watu milioni 50 duniani

UM umezindua ombi kuwasaidia watu milioni 50 duniani

Umoja wa Mataifa unaomba dola bilioni 7.4 ili kukidhi gharama za operesheni zake za kibinadamu kwa mwaka 2011.

Fedha hizo zinatarajiwa kushughulikia matatizo makubwa 14 ya kibinadamu duniani kote ambako watu zaidi milioni 50 wameathirika. Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valarie Amos anasema vita na majanga ya asili bado yanatawala maisha ya watu wengi katika nchi zilizoathirika, yakiwalazimisha kuzihama nyumba zao huku wakikosa huduma muhimu kama maji ya kunya na huduma za afya.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)

Nchi 28 zitanufaika na ombi hilo la msaada wa 2011.Sudan ndio itakayopata sehemu kubwa ya fedha hizo dola bilioni 1.7, ikifuatiwa na Haiti ambayo itapokea dola milioni 907 na kisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo itapata dola milioni 719.