Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filosofia inajenga amani na maelewano:Ban

Filosofia inajenga amani na maelewano:Ban

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya filosofia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO unatoa fursa ya mitazamo ya filosofia kuweza kupatikana kwa urahisi kwa maprofesa, wanafunzi, wanazuoni, wadogo kwa wakubwa na jamii kwa ujumla.

Nia ya kufanya hivyo ni kutoa nafasi ya kuchagiza fikra na mijadala kuhusua masuala mbalimbali katika jamii. Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema filosofia inatusaidia kuelezea sisi ni nani na mahusiano tuliyonayo miongoni mwetu na dunia tunayoishi.

Amesema kuanzia mmifumo ya imani na ustaarabi hadi maadili mapya ya udaktari utafiti wa filosofia unaendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya binadamu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanahusisha pia mwaka wa kimataifa wa mahusiano ya tamaduni ambao ni mradi wa UNESCO. Pia yameangukia katika mwaka wa kimataifa wa vijana ambao unapigia upatu majadiliano na utengamano katika jamii. Amesema tutambue jukumu la filosofia katika dunia ya sasa iliyounganishwa na mambo mengi.