Ban amesisitiza kutimiza malengo ya milenia barani Afrika

10 Juni 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye anaendelea na ziara barani Afrika amessisitiza umuhimu wa kutimiza malengo ya milenia.

Ban aliyekuwa akizungumza na bunge mjini Younde Cameroon baada ya kukutana na Rais Paul Biya wa nchi hiyo na viongozi wengine wa serikali, amesema bara la Afrika linaweza kufikia malengo ya milenia. Pamoja na juhudi za bara hilo amesema mataifa tajiri lazima yatimize ahadi za kuongeza mara mbili msaada kwa Afrika, ahadi ambazo wamezitoa mara kadhaa kwenye mikutano ya nchi nane tajiri duniani G-8, mikutano ya G-20 na kwenye Umoja wa Mataifa.

Amesema ili kutimiza malengo hayo juhudi za pamoja zinahitajika, kutoka kwa serikali, wahisani, jumuiya za kijamii, sekta binafsi na Umoja wa Mataifa.

(SAUTI BAN MDG'S)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter