Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wachukulieni wanaokimbia vita kuwa ni wakimbizi-UNHCR

Wachukulieni wanaokimbia vita kuwa ni wakimbizi-UNHCR

Kukiwa na idadi kubwa ya watu waliotawanywa kutokana na sababu mbalimbali duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, sasa limeondoka katika kuhimiza ulinzi kwa wakimbizi kimataifa na kutoa mwongozo mpya, wa kushughulikia watu wanaokimbia nchi zao kwa sababu ya vita.

Muongozo huo una lengo la kuhakikisha kwamba nchi zote duniani zinawachukulia wanaokimbia vita na machafuko mengine kuwa ni wakimbizi. Vannina Maestracci  [Mestrach] ni msemaji wa UNHCR Geneva.

(SAUTI YA VANNINA)

“kuna tofauti linapokuja suala la kuamua uhakiki wa wakimbizi, na baadhi ya nchi hazitambui waathirika wa unyanyasaji kama wanawezekana kuwa wakimbizi”.