Watu wenye ulemavu wajumuishwe kwenye maendeleo Ban
Lazima jamii ikomeshe ubaguzi na kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika maendeleo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake kuhusu siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu inayotarajiwa kuadhimishwa terehe tatu Disemba hapo kesho.
Ban amesema agenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu SDGs, inapigia chepuo kutoachwa nyuma kwa mtu yeyote na kwamba ili kutimiza hili watu wenye ulemavu wanahitaji kujumuishwa vilivyo katika jamaii na maendeleo.
Ametaka mamlaka za kitaifa na serikali za mitaa, wafanya biashara na wadau wote wa kijamii kuimarisha juhudi za kukomesha ubaguzi na kuondoa vikwazo vinavyowazuia watu wenye ulemavu kupata haki zao kisiasa, kiuchumi kijamii na kiutamaduni.
Katibu Mkuu ametaka jamii kuhakikisha ushiriki wa kundi hilo na kuzingatia ubinadamu na kuchangamana.