Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 JULAI 2024

15 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya harakati za chanjo kwa watoto na ulinzi wa amani na usalama inaozingatia haki za binadamu nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Rwanda, kulikoni?

  1. Viwango vya chanjo za utotoni ulimwenguni kote vilikwama mwaka 2023 na kuacha watoto milioni 2.7 bila chanjo au kupata kiwango kisichotosheleza cha chanjo ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu za ripoti mpya zilizochapishwa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  duniani UNICEF
  2. Maafisa wa polisi wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wametoa mafunzo kwa askari polisi wa nchi hiyo ili waweze kuimarisha ulinzi na usalama wakati huo huo wakiheshimu haki za binadamu.
  3. Katika makala Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Tanzania limefanya kikao kazi cha maandalizi ya kutengeneza Mradi wa maendeleo ya mifumo ya chakula katika nyanda za juu kusini maeneo ya Bonde la Usangu pamoja na visiwani Zanzibar.
  4. Na mashinani Prince ISHIMWE mwanafunzi wa Shule ya ufundi ya Forever TSS nchini Rwanda anatueleza jinsi uunganishwaji wa intaneti shuleni unamsaidia kuwasiliana na  kushirikiana  na wanafunzi wenzake katika  kujifunza na kuafanya utafiti mtandaoni.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'34"