22 JULAI 2020
Katika Jarida la Habari za UN hii leo Flora Nducha anakuletea
-Mkimbizi kutoka Afghanistan aliyepatiwa hifadhi katika kijiji kimoja nchini Ufaransa sasa alipa fadhilia kwa kutumia talanta yake ya ufundi cherahani, anashona barako na kuzigawa bure kwa jamii inayomuhifadhi
-Mafunzo ya ujasiriliamali yanayotolewa na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD kwa kushirikiana na serikali ya Norway na Niger yaleta nuru kwa vijana wakimbizi mjini Diffa Niger
-Nchini DRC kutaka na mtoto wa miaka 7 ambaye ni mkulima wa bustani anasema analinda mazingira lakini pia kusaidia kulisha familia yake
-Makala yetu inatupeleka Tanzania kumulika vijana na masomo ya masuala ya anga ikiwemo uhandisi, urubani na kuongoza ndege
-Na mashinani tutakuwa kenya kwa msichana ambaye anaelimisha wachuuzi kwenye makazi ya Kibera kuhusu kujilinda na COVID-19