Mradi kabambe wa kukabiliana na hali ya jangwa kwenye ukanda wa sahel na Sahara wa Great Green Wall, GGW umepokea ufadhili wa dola bilioni 14.236 za kimarekani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Msataifa leo amelaani vikali shambulio la kisu lililofanyika ndani ya kanisa kwenye mji wa Kusini wa Nice nchini Ufaransa ambalo limesababisha vifo vya waumini watatu.
Katika Jarida la Habari za UN hii leo Flora Nducha anakuletea
-Mkimbizi kutoka Afghanistan aliyepatiwa hifadhi katika kijiji kimoja nchini Ufaransa sasa alipa fadhilia kwa kutumia talanta yake ya ufundi cherahani, anashona barako na kuzigawa bure kwa jamii inayomuhifadhi
Kutana na mkimbizi Hamidullah mwenye umri wa miaka 23. Baada ya kukimbia machafuko Afghanistan na kupokelewa na kukirimiwa na Kijiji cha Pessat-Villeneuve nchini Ufaransa kwa msaada wa shirika la Umoja wa sasa analipa fadhila kwa kuisaidia jamii inayomuhifadhi kupambana na janga la corona au COVID-19.
Ujerumani na Ufaransa leo zimesisitiza uungaji mkono wa kisiasa na kifedha kwa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO wakati huu ambapo janga la virusi vya Corona au COVID-19, limeendelea kutikisa ulimwengu.
Wakimbizi 183 waliotokea Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na kusaka hifadhi nchini Chad , leo wamewasili Ufaransa kwa ajili ya makazi mapya kupitia mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.
Kuzuia vyanzo vote vinavyosababisha uvunjifu wa amani duniani ndio dawa mujarabu ya kulinda na kudumisha amani ya dunia kuliko kukabili machafuko wakati yameshatokea. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini Paris Ufanransa hii leo, wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa la Paris kwa ajili ya amani.
Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac amefariki dunia hii leo ambapo kufuatia taarifa za kifo chake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema taifa hilo la Ulaya limepoteza mmoja wa viongozi wake muhimu waliokuwa mstari wa mbele kusongesha demokrasia ya ushirikiano wa kimataifa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne jijini New York, Marekani akitaka mwelekeo wa kijasiri zaidi katika kutatua vitisho vikubwa vinavyokabili dunia hivi sasa.