Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UNEP/Nicholas Greenfield

Ombi la dola milioni 267.5 litasaidia katika kukabiliana na COVID-19 Kenya

Serikali ya Kenya, Umoja wa Mataifa na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wametoa ombi la dharura la dola milioni 267.5 kwa ajili ya kukabiliana na mahitaji ya sasa na ya dharura kwa zaidi ya watu milioni 10. Taarifa kamili na Jason Nyakundi 

(Taarifa ya Jason)

Ombi hilo liliotolewa jijini Nairobi, Kenya linalenga kuchagiza ufadhili wa dharura kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia katika kusaidia serikali kukabiliana na mlipuko wa wa ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19.

Sauti
2'46"