Hata sisi wachora vibonzo, COVID-19 imeathiri kazi zetu-Nathan Mpangala
Hata sisi wachora vibonzo, COVID-19 imeathiri kazi zetu-Nathan Mpangala
Nathan Mpangala ni mchoraji maarufu wa vibonzo wa nchini Tanzania ambaye anasema tayari kwa namna fulani ameanza kuona athari za mlipuko wa virusi vya corona katika kazi zake, "Mimi ni mmoja wa waathirika kwa sababu nimebadilisha ule utendaji kazi wa kila siku, ni kweli kwamba sisi wachoraji wengi tunakuwa na ofisi za kutekeleza kazi zetu au ni waajiriwa. Mimi nafanya kazi na vyombo vya habari na wakati mwingine nalazimika kwenda kwenye vyomba vya habari lakini kwa kuwepo virusi vya corona sasa kwenda ofisini ni pale tu kunapo ulazima mkubwa."
Ukurasa kuhusu virusivyacorona & taarifa mpya
Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa. Kwa habari mpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.Bwana Mpangala anasema hivi sasa kwa kuwa anatekeleza agizo la kutokukutana na watu wengi ili kujikinga na ugonjwa, analazimika kutumia mitandao ya kijamii ili kupata mawazo ya kazi zake, "ninategemea mandao kuangalia na wengine kwa mfano wachoraji kutoka nje wanafanya nini kwa mfano kuhusu corona alafu kutoka pale napata mawazo ya kuendeleza kazi zangua."