Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN, mdau wa Kenya katika vita dhidi ya COVID-19: Mratibu Mkazi Kenya

Umoja wa Mataifa unashirikiana kwa karibu na serikali ya Kenya kusaidia kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona, au COVID-19.
Na Siddharth Chatterjee, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya

Mshikamano, matumaini na ushirikiano vyahitajika kukabili COVID-19: Guterres

Wakati hofu ikiendelea kutanda kote duniani kufuatia kusambaa kwa mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “sasa kuliko wakati mwingine wowote tunahitaji mshikamano, tumaini na utashi wa kisiasa ili kukabiliana na janga hili kwa pamoja.”

Afrika ni wakati wa kuamka na kujiandaa na zahma ya COVID-19:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa wito kwa bara la Afrika kuamka na kujiandaa na tishio kubwa la kimataifa za mlipuko wa virusi vya Corona , COVID-19. Katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari mjini Geneva mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus amesema “kitu muhimu na bora kwa Afrika ni kujiandaa kwa zahma na kujiandaa sasa”

Uelewa wa COVID-19 na mbinu za kujikinga miongoni mwa wakazi, Pangani, Tanzania

Wakati visa vya ugonjwa wa COVID-19 vikiongezeka duniani kote na sasa pia Afrika Mashariki ikiwemo nchini Tanzania. Je wananchi wanaelewa vipi kuhusu virusi vya coroan na wamechukua hatua zipi kujikinga dhidi ya virusi hivyo?

Sauti -
2'51"

Tuko pamoja na serikali ya Sudan Kusini katika vita dhidi ya COVID-19:UN

Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umetangaza hatua mpya katika kusaidia juhudi zinazoongozwa na serikali ya Sudan kusini katika kuzuia na kujiandaa na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19. Grace Kaneiy ana ripoti kamili.

Sauti -
1'46"

Tanzania visa vya COVIDI-19 vyaongezeka, wafanyabiashara wateta

Nchini Tanzania  maambukizi ya virusi vya Corona au COVID-19 yameendelea ambapo hii leo wagonjwa wapya wawili wote wakazi wa Dar es salaam wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo baaada ya mmoja kuingia nchini kutoka safari ya Denmark, Uswisi na Ufaransa huku mwingine akiwa amerejea kutoka Afrika Ku

Sauti -
2'7"

Uganda yajihadhari kabla ya shari ya COVID-19

Serikali ya Uganda imechukua hatua ya kufunga shule zote, masoko na mijumuiko yote ya umma kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19 kwenye nchi hiyo ambayo yenyewe hadi sasa haina mgonjwa hata mmoja lakini imezungukwa na nchi mlimothibitishwa mlipuko wa virusi hivy

Sauti -
2'24"

19 MACHI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Licha ya kutokuwa na mgonjwa hata mmoja wa COVID-19 serikali ya Uganda imefunga shule zote hadi vyuo vikuu katika maandalizi ya kupambana na mlipuko endapo utazuka ugonjwa huo

Sauti -
12'32"

Uganda yafunga shule zote kuzuia hatari ya COVID-19

Serikali ya Uganda imechukua hatua ya kufunga shule zote, masoko na mijumuiko yote ya umma kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19 kwenye nchi hiyo ambayo yenyewe hadi sasa haina mgonjwa hata mmoja lakini imezungukwa na nchi mlimothibitishwa mlipuko wa virusi hivyo. 

COVID-19 Tanzania: Wafanyabiashara ndogo ndogo wazungumza

Nchini Tanzania  maambukizi ya virusi vya Corona au COVID-19 yameendelea ambapo hii leo wagonjwa wapya wawili wote wakazi wa Dar es salaam wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo baaada ya mmoja kuingia nchini kutoka safari ya Denmark, Uswisi na Ufaransa huku mwingine akiwa amerejea kutoka Afrika Kusini.